Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maelfu ya Waumini Nchini Iraq, leo hii Ijumaa (20-06-2025) wamejitokeza kwa wingi kutekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa katika Mji wa Sadr, Baghdad, huku wakipaza sauti zao za kauli mbiu dhidi ya Marekani na Utawala Haram wa Kizayuni.
Hii ni Ijumaa ya Ghadhabu na Ushindi dhidi ya adui mzayuni aliyeamua kuanzisha vita vya kiuchokozi visivyo vya haki dhidi ya Iran, ambapo hivi sasa Dunia imeshudia na adui mwenyewe ameshuhudia uwezo mkubwa wa Kijeshi wa Iran baada ya Iran kuja Majibu Makali ya Kijeshi kwa kuvurumisha Makombora hatari zaidi katika Operesheni ya "Ahadi ya Kweli 3".
Israel imeanza kuomba Msaada wa Marekani kuingilia vita hii, na hii ni kwa sababu imevuna ilichopanda baada ya kukutana na Kisasi chenye Nguvu toka Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Tunatumaini Utawala haram wa Kizayuni - Israel, utaangamizwa hivi karibuni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Your Comment